Kujua kama mtu ameku-block katika mtandao wa Instagram, unatakiwa kujaribu ku-search akaunti yake.
- Kama huioni akaunti yake au hauoni profile picture yake, basi huenda huyo mtu ameku block.
- Instagram hawakutumii taarifa kama kuna mtu ameku block.
Karibu tena BongoTechno.com kupeana mawili matatu kuhusu teknolojia. Katika makala ya leo nitakufundisha jinsi ya kugundua kama mtu ameku-block katika mtandao wa Instagram.
Hivi ushawahi kujiuliza najuaaje kama mtu ameni-block Instagram? Au nini kinatokea kama mtu ameni-block?
Kama unaona hivi karibuni huoni posts za mtu au stories zake, au kutokumuana aki-react katika posts zako, basi kuna mambo mawili, aidha hajaingia kwa mda au hajapost kwa mda au ameizima akaunti yake, kama sivyo basi ameku-block.
Jinsi ya kujua kama mtu ameku-block Instagram
Fuata hatua hizi chache ili kujua kama mtu fulani ameku-block;Kwanza, i-search hiyo akaunti unayodhani imeku-block kupitia App yako ya Instagram.
- Kama hiyo account ni private na huioni, basi itakuwa ume-blockiwa.
- Kama hiyo account ni public, na ukiitembelea huoni profile picture, namba za post, follower na watu aliowa-follow, na pia kwa upande wa post unakuta umeandikiwa "No Posts Yet", basi jua ameku-block.
Unaweza kujithibishia hilo kwa 100% kwa kufanya uhakiki wa mwisho ambao ni rahisi kabisa, fanya hivi :
Tumia account nyingine ya Instagram, kwa mfano account ya rafiki yako...... kisha m-search huyo mtu unayedhani ameku-block, na kama ukimuona basi jua ameku-block katika akaunti yako.
Hizo ndizo njia rahisi za kujua kama mtu ameku-block katika mtandao wa Instagram.
Soma Pia : Jinsi ya kutumia WhatsApp bila namba ya simu
Ungana nasi Instagram @ BONGO TECHNO
Wasiliana Nasi == > bongotechno@gmail.com