Instagram ni mmoja wa mitandao maarufu sana duniani na ni mtandao unaopendwa zaidi. Mpaka kufikia sasa mtandao huu una watumiaji zaidi ya watu milioni 500 duniani.
Watu hutumia mtandao huu kuangalia picha, video, kufuatilia habari mbalimbali zinazotrend na pia kujifunza mambo mbalimbali. Na pia watu wengine hutumia mtandao huu kuendesha biashara zao kutokana na kuwa na watumiaji wengi hivyo kuna nafasi kubwa ya kuuza bidhaa zao au huduma zao.
Ukiachana na hayo yote, kuna sababu zingine mbalimbali ambazo zinamfanya mtu achukue mapumziko kwa mda fulani kutotumia mtandao huo. Kama unataka mapumziko ya muda ya mtandao huu, au unataka tu akaunti yako isionekane kwa muda katika mtandao huu kutokana na mambo mbalimbali, basi njia moja wapo ni kuizima akaunti yako ya Instagram.
Unapoizima akaunti yako ya Instagram, akaunti yako inakuwa haionekani, posts zako zote zinakuwa hazionekani popote pale mpaka pale utakapoamua kuirudisha mwenyewe. Katika makala hii bongotechno.com tutakufundisha hatua zote za jinsi ya kuizima akaunti yako kwa muda. Fuata hatua hizi chini uweze kufanya hivyo.
Jinsi Ya Kuzima (ku-disable / deactivate) akaunti yako ya Instagram
Kwanza kabisa unatakiwa kufahamu kwamba huwezi kuzima akaunti yako kupitia App ya Instagram. Hivyo unalazimika kutumia browser kama vile Chrome n.k
1. Fungua browser yako
2. Andika www.instagram.com
3. Kisha Log in katika akaunti yako.
4. Ukisha log in utabonyeza profile picture yako upande wa kulia.
5. Kisha utabonyeza Edit Profile
6. Utashuka chini, kisha utabonyeza Temporarily disable my account upande wa kulia.
7. Utachagua option utapoulizwa kwanini unataka kuzima akaunti yako (Why are you disabling your account?) na kisha utaingiza tena password yako. Ukishachagua sababu na kuingiza password ndipo utaona option ya ku disable account yako.
8. Mwisho utabonyeza Temporarily Disable Account
Hapo utakuwa umefanikiwa kuizima akaunti yako ya Instagram.
Kumbuka : kwa kufuata hatua hizo hapo juu akaunti yako utakuwa umeificha. Hakuna atakayeweza kuiona akaunti yako wala posts zako.